Jina lake kamili ni Ali Suleiman Ali. Amezaliwa mwaka 1992 Zanzibar katika kisiwa cha Pemba. Kabila lake ni Al-Salmi. Jina kamili la baba yake ni Suleiman Ali Hamoud na mama yake ni Fresha Sultan. Ni mtoto watatu
Elimu yake ya msingi aliipata mkoani Tanga katika shule ya msingi Makorora na baadae alijiunga na shule ya sekondari Usagara Tanga.
Elimu yake ya kidato cha 5 na 6 aliipata visiwani Zanzibar katika shule ya UTAANI SEC HIGH SCHOOL. Baada ya kufaulu vyema alifanikiwa kujiunga na chuo kikuu cha Dar es salaa(UDSM) lakini kutokana na matakwa ya familia yake walimuhamisha na kumpeleka chuo kikuu cha DODOMA(UDOM) ambako anaendelea na masomo yake ya kuhitimu shahada ya kwanza.
Shuguli ya uandishi wa hadithi aliianza wakati akiwa kidato cha 3 ambapo kwa kipindi hicho aliandika kazi nyingi ambazo hakufanikiwa kuziweka sokoni kutokana na umri wake ulikuwa mdogo sana kiasi ambacho kila mtu angemshangaa kwa kitendo hicho.
Alipojiunga na kidato cha 5 hadi cha 6 alifanikiwa kuandika riwaya iliyoitwa TAMBIKO pamoja na KELELE ZA MKIWA ambazo hakuzitoa sokoni kwa sababu zake binafsi.
"Sikupenda kuzitoa kazi hizo kwa sababu ambazo mimi mwenyewe nazielewa, sipendi kuweka wazi..." Alijibu hivyo.
Akiwa mwaka wa pili baada ya kujiunga na chuo kikuu ndipo aliitoa sokoni riwaya yake ya DHAMBI YA MOYO na ilimvutia kila mtu. Riwaya hiyo ndio imemtengezea jina na umaarufu mkubwa hadi kwa waandishi wakubwa nchini Tanzania kama vile Hussein Issa Tuwa na wengineo.
Kwasasa anatarajia kuiachia sokoni Riwaya yake nyengine iitwayo NCHI YA URITHI.

MASUALI ALIYOULIZWA NA KUYAJIBU
1) Ulifikiria nini hata uliamua kuandika riwaya yako ya DHAMBI YA MOYO ambayo imekuwa ya mvuto kwa kila mtu? JIBU: "Niliichunguza jamii"
2)Ni nani amabaye anakusapoti nakukupa dira katika kaai zako? JIBU: " Ni wazazi wangu pamoja na baadhi ya waandishi mashuhuri nchini "
kama nani? JIBU: " Hussein Issa Tuwa, Ibrahim Gama na wengineo"
3) Umeoa? JIBU: " Bado sijalifanya hilo "
kwanini? JIBU: " hahahaha usiwe na wasiwasi"
Huyo ndie ALI SULEIMAN ALI, mwandishi wa riwaya ya DHAMBI YA MOYO. Kwa maswali pamoja na ushauri au maoni wasiliana nae kupitia barua pepe Salmybomu05@Gmail.com
No comments:
Post a Comment