SAFARI YENU
Sio hoja wala tija kwa wingi wenu.
Yawezasimama kauli au tendo la peke yake likawa na tija mbele ya Mungu muweza.
Anzeni sasa, munasubiria nini? Mbona kimya kikubwa. Hamukumzowesha hivyo. Muliyabeba matofali ya nyumba mbovu na
kumtupia kichwani bila sababu. Hakustahiki kubaki hai. Shangaeni sasa au
hamumuoni?.
Muliwauwa watoto wachanga miaka ilee
ya marehemu babu yangu, mukahifadhi NDERE
ndani ya mifuko yenu. Wapya waliozaliwa na walezi wao wasiowazaa mukawarambisha
NDERE hiyo ya siri, walikuwaje?. Waoneni
kwa macho yenu. Mwema akawa mbaya. Mulimuhofia kwa mabadiliko?. Sielewei, ALIZINI?. Jicho la tatu limekufa, musilitegemee.
Muliipanga safari peke yenu,
mukamkabidhi yaliyo mioyoni mwenu kwa kumtupia chini. EENHH!!! Shupavu nyinyi!.
Mulimgeukia alipokataa kuramba unga wenu. HAMUKUMSACHI?.
Alikuwa na ule wa RUTUBA anaubugia
peke yake, unaangaza dunia.
Alijinadi na kusema “Haya njooni WATUMWA. Naona yaliyomo ndani ya nafsi
zenu bila ya kujielewa. Poleni. Kuleni tena NDERE kidogo. Tafadhali musianguke chini ya miguu yangu. Teteeni
huo. Siwalazimishi kuramba wakwangu. Poteeni, WAONEVU wakubwa”. Alighairisha kikao mwalimu Abasi baada ya
kuwaeleza hayo. Walijisuta na kuanza kuondoka.
ALI S. ALI

No comments:
Post a Comment